Tanzania / Machi 25, 2018 / Mwandishi: Rasimu / Chanzo: Zanzibar24
Serikali ya mapinduzi zanzibar imesema itaendelea najitihada zake za kuimarisha sekta ya elimu hususan elimu ya vyuo vikuu kwa lengo la kukuza uchumi na maendeleo ya taifa .
Waziri wa biashara na viwanda zanzibar mhe balozi Amina Salum Ali ameyaeleza hayo wakati akizungumza na wana funzi wa chuo cha utawala wa umma tunguu katika sherehe za siku ya serekali ya wanafunzi wa chuo hicho ( zipaso day).
Amesema ili taifa liweze kukabilana vyema na kasi ya ukuaji wa uchumi linahitaji kupata wataalam waliobobea kupitia fani mbali mbali zikiwemo za kibiashara hivyo serekali haitasita kuongeza kasi ya uimarishaji wa sekta hiyo ili kuona kwamba wananchi wake na hasa vijana wanaingia katika soko la ajira na kuweza kufikia malengo.
Hivyo balozi Amina amewataka vijana na watumishi wa umma kuzichangamkia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na kujiunga na vyuo kujiongezea taluma ili kuweza kuleta mafanikio.
Aidha ameutaka uongozi wa chuo hicho kuendelea kutoa elimu bora hasa kwa watumishi wa umma ili watapotoka hapo waweze kulitumikia vyema taifa na kuleta maslahi kwa jamii.
Nao katika risala yao wanafunzi hao wamesema licha ya mafanikio waliyoyapata lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali zikiwemo uhaba wa vitendeakazi,uhaba wa vifaa vya matibabu na dawa katika sehemu ya afya ,uchache wa vitabu ,na ukosefu wa uzio katika eneo la chuo.
Chanzo cha Habari:
http://zanzibar24.co.tz/2018/03/15/smz-yaahidi-kuendelea-kuimarisha-sekta-ya-elimu-ya-juu/