Tanzania: SMZ yaahidi kuendelea kuimarisha Sekta ya elimu ya juu

Tanzania / Machi 25, 2018 / Mwandishi: Rasimu / Chanzo: Zanzibar24

Serikali ya mapinduzi zanzibar imesema itaendelea  najitihada zake za kuimarisha  sekta ya  elimu hususan  elimu ya vyuo vikuu kwa lengo la kukuza uchumi na maendeleo ya taifa .

Waziri wa biashara na viwanda  zanzibar mhe balozi Amina Salum Ali  ameyaeleza  hayo wakati  akizungumza  na wana funzi wa chuo  cha utawala wa umma tunguu katika  sherehe za siku ya serekali  ya wanafunzi  wa chuo hicho  (  zipaso day).

Amesema ili taifa liweze kukabilana vyema na kasi ya ukuaji wa uchumi  linahitaji kupata  wataalam waliobobea kupitia fani mbali mbali zikiwemo za kibiashara  hivyo serekali haitasita  kuongeza kasi ya uimarishaji wa sekta hiyo ili kuona kwamba wananchi wake na hasa vijana wanaingia  katika soko la  ajira  na kuweza kufikia malengo.

Hivyo balozi Amina amewataka vijana  na watumishi wa  umma  kuzichangamkia fursa  zilizopo ikiwa ni pamoja  na kujiunga  na vyuo  kujiongezea taluma  ili kuweza  kuleta mafanikio.

Aidha  ameutaka  uongozi wa  chuo  hicho kuendelea kutoa elimu bora  hasa kwa watumishi  wa umma ili watapotoka hapo waweze kulitumikia  vyema taifa  na kuleta maslahi kwa jamii.

Nao katika risala yao wanafunzi  hao wamesema licha ya mafanikio waliyoyapata  lakini bado wanakabiliwa na changamoto  mbali mbali zikiwemo  uhaba wa vitendeakazi,uhaba wa vifaa vya matibabu na dawa katika sehemu ya afya ,uchache wa vitabu ,na ukosefu wa uzio katika eneo la chuo.

Chanzo cha Habari:

SMZ yaahidi kuendelea kuimarisha Sekta ya elimu ya juu

Comparte este contenido: