Tanzania / Aprili 22, 2018 / Mwandishi: mik-dadi / Chanzo: Zanzibar 24
Baadhi ya Wazazi na Walezi wa Mkoa wa Kusini Unguja wameiomba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwachukulia hatua za kisheria walimu wanaokataa kuwapokea wananfunzi wenye ulemavu katika skuli ili wanafunzi hao waweze kunufaika na elimu.
Wakizungumza na Zanzibar24 kwa maskitiko makubwa kwa niaba ya wananchi hao Mwenyetiti wa watu wenye Ulemavu Wilaya ya Kati Yunus Kassim na Mratibu wa wanawake na watoto Shehia ya kikungwi Bahati Issa wamesema kumejitokeza tabia kwa baadhi ya Walimu kuwakaa wanafunzi wenye ulemavu wakati wanapoenda kuandikishwa.
Wamesema kila mwananchi ana haki ya kupata haki zao za msingi hivyo wanashangazwa na baadhi ya walimu kuwakataa wanafunzi hao bila ya wananchi kujua sababu za msingi za kukataliwa kwa watoto wao.
Wamesema wakati umefika kwa maafisa Elimu kufatilia skuli ambazo zinaendelea na tabia hiyo ili walimu waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na watoto waweze kunufaika na haki zao za kupata elimu katika nchi yao.
Aidha wametowa wito kwa Wizara ya Elimu na Mfunzo ya amali Zanzibar kuwapa mafunzo walimu ya kuwasomesha wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususani wenye ulemavu wa kusikia katika skuli ili wanafunzi hao waweze kufahamu wanachosomesha wakiwa madarasani.
Kwa upande wake Afisa Elimu na Mafunzo ya amali Mkowa wa Kusini Unguja Abdallah Makame Makame amewaka Wazazi hao kuripoti katika Ofisi yake yanapotokeza matatizo hayo ili walimu waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema mapka sasa hakuna kesi iliyoripotiwa lakini wazazi hao wanaendelea kulalamika mitaani jambo ambalo ni kinyume na sheria na wanasababisha watoto wao kutopata haki zao za misngi katika elimu.
Amesema azma ya serikali ni kuona kila mwananchi ananufaika na haki zake za msingi ikiwemo kupata matibabu na elimu hivyo si vyema kwa wazazi na walezi kuendekeza muhali katika kuwaripoti walimu wanaokiuka majukumu yao kwa wanafunzi.
Chanzo cha Habari:
http://zanzibar24.co.tz/2018/04/17/wazazi-na-walezi-wameiyomba-serikali-kuwachukulia-hatua-za-kisheria-walimu/