Tanzania: wizara ya elimu imewataka walimu nchini watakiwa kujiendeleza kitaaluma

Tanzania / Februari 25, 2018Mwandishi: Chanzo: zanzibar24

Wizara ya  elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar imewataka walimu nchni kujiendeleza kitaaluma ili kutoa elimu inayoendana  na mahitaji ya wanafunzi  katika kuengeza ufaulu wa masomo yao.
 Akizungumza katika mkutano uliyowakutanisha wadau wa sekta ya elimu katika kujadili tathmini ya masomo kwa mwaka mzima, Kaimu waziri wa Wizara ya Elimu Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amesema fani ya elimu imekuwa ikishushwa hadhi kutokana na baadhi ya walimu kushindwa kujiendeleza kitaaluma.
Amesema imefika wakati kwa walimu kujua umuhimu wa kazi zao katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi ili waweze kunufaika na elimu inayotolewa katika skuli pamoja na kuengeza kasi ya kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali Nchi.
Aidha Kaimu kombo ametowa wito kwa Wazazi kuengeza kushirikiana na walimu katika kufatilia maendeleo ya wanafunzi ili kuwaengezea walimu ari ya kusomesha jambo ambalo litasaidia kurejesha hadhi na heshima ya walimu Nchini.
 Kwa upande wake Mwakilishi wa mtandao wa Elimu Zanzibar khamis Saidi ametowa wito kwa serikali kuwashirikisha wadau wa sekta ya elimu katika kuandaa bajeti ya sekta hiyo ili bajeti hiyo iweze kutumika kwa mahitaji yaliyokusudiwa .
Aidha amesema sekta ya elimu inahitaji mashirikiano mazuri baina ya serikali na wadau wa maendeleo ili kujua namna ya kuengeza ufaulu kwa wanafunzi.
 Nae mwakilishi kutoka Shirika la kuhudumia watoto nchini UNICEF Masoud Muhammed amesema wataendelea kuuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua matatizo yanayo ikabilia sekta ya elimu.
Amesema mpaka sasa kuna matatizo mbalimbali ambayo yansababisha wananfunzi kutopata elimu ipasavyo ikiwemo wingi wa wananfunzi madarasani.
Amesea tatizo hilo pia la waingi wa wananfunzi maskulini linachangi baadhi ya wananfunzi kutoandikishwa skuli na wazeee wao jambalo ambalo linachangia kupotea kwa haki za watoto hao.
Mkutano huo wa siku tatu unaendelea kufanyika mazizini imekusudia kufanya tathmini ya mwaka katika sekta ya elimu ili kujua namna ya kupunguza matatizo yanayoikabilia sekta hiyo.
Chanzo cha Habari:
http://zanzibar24.co.tz/2018/02/19/wizara-ya-elimu-imewataka-walimu-nchini-watakiwa-kujiendeleza-kitaaluma/
Comparte este contenido: