Tanzania / Mei 20, 2018 / Mwandishi: Wahariri wa Watumishi / Chanzo: Nijuze
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezipongeza shule za sekta binafsi kwa ulipaji mzuri wa kodi na kutambua umuhimu wake katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Hayo yamezungumzwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ole Nasha ameeleza kuwa kwa kutambua ushirikiano ulipo na sekta binafsi imekuwa ikiondoa changamoto zinazowakabili wamiliki wa shule hizo kama kuondoa kodi na tozo mbalimbali.
“Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kubora mazingira ya wao katika elimu, tutaendelea kuboresha zaidi ili wafanye kuwekeza kwa kiurahisi lakini vile vile naomba niseme kwamba sekta binafsi wamekuwa walipaji wazuri wa kodi na wanatambua umuhimu wa kulipa kodi katika maendeleo ya Taifa kwa hiyo na kwamba tupo pamoja katika kukabiliana nao kuhusiana na namba ya kuweza kuangalia namna ya kupunguza hizo kodi bado tunasisitiza kwamba ni vizuri tukaendelea kushirikiana ili kuhakikishia baadhi ya gharama ambazo ni mhimu ziweze kulipwa na wale ambao wanaweza kuchangia”
Aidha, serikali imedai bado inatambua vizuri kabisa umuhimu wa sekta binafsi katika utoaji wa elimu ili kuhakikisha mazingira rafiki katika utoaji wa elimu, serikali imejizatiti kufanya majadiliano na sekta binafsi kwa lengo la kuondoa changamoto zinazowakabili hadi sasa serikali imefanikiwa kuondoa kodi na tozo mbalimbali ambazo awali walikuwa wakitozwa wamiliki wa shule binafsi.
Chanzo cha Habari:
http://www.nijuze.co.tz/kitaifa/nasha-serikali-kushirikiana-na-sekta-binafsi-kuboresha-elimu/